Gunze Luhangija, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) aliyekuwa akisomea Shahada ya Menejimenti ya Ushirika na Uhasibu (BCMA), amekutwa amejinyonga huku chanzo kikisemekana ni kutokana na msongo wa mawazo uliosababishwa na kukataliwa na mpenzi wake aliyekuwa anamgharamikia ikiwemo kumpangishia nyumba na kumnunulia simu aina ya iPhone 14.
![]() |
Picha kutoka maktaba |
Ingawa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro bado linachunguza kiini cha kifo hicho, inaelezwa msongo wa mawazo uliosababishwa na kuvunjika kwa mahusiano yake na mpenzi wake, umechangia hatua hiyo.
Baada ya Makamu Mkuu wa Chuo cha MoCU, Profesa Alfred kutoa tangazo la kifo hicho kilichotokea Januari 7, baadhi ya wanafunzi chuoni hapo walisema huenda mapenzi yamechangia kwani marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake.
“Huyu kijana hapa chuo katusononesha sana wana Mwanza. Siku ya Boxing Day alimnunulia demu (mpenzi) wake iPhone 14 (simu) na baada ya siku chache demu akamkataa kwamba kapata mtu mwingine...dogo kajitundika,” zilieleza taarifa hizo.
Gunze, aliyekuwa akisoma shahada ya menejimenti ya ushirika na uhasibu (BCMA) mwaka wa pili, anadaiwa kujinyonga huko Mto Rau katika Manispaa ya Moshi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo alithibitisha tukio hilo na kusema jeshi linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo.
KAMA HUKUTAZAMA VIDEO HII BOFYA SASA KUTAZAMA