Mwanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, aliyetoweka wikendi iliyopita, alipatikana amefariki katika nyumba ya mpenzi wake mtaa wa Kahawa Wendani, Kaunti ya Kiambu nchini Kenya.
USIPITWE NA VIDEO HII MUHIMU KWA MWAKA 2023
Imeelezwa kuwa jioni ya siku hiyo baada ya mwanafunzi huyo kukawi kurejea nyumbani wazazi waliamua kumpigia dada yake simu kujua ikiwa atalala kwake lakini hata hivyo hakuwa amefika pia kwake.
Baada ya siku chache harufu iliyokuwa ikitoka katika chumba cha mpenzi wake kiliwashtua majira ambao baada ya kutoa taarifa na kufungua chumba hicho walikuta mwili wa mwanafunzi huyo.
“Mwanamume anayeishi hapo hakuwepo na tuligundua kuwa kulikuwa na harufu mbaya kutoka kwa nyumba. Ilinuka kama kitu kilichooza ndani ya nyumba iliyofungwa,” jirani alisema.
Jeshi la polisi katika Kaundi hiyo wameanzisha uchunguzi na kumsaka mpenzi wa msichana huyo ambaye alitokomea baada ya mkasa huo.