MWANAMKE AUAWA KISHA WAUAJI KUONDOKA NA SEHEMU ZA SIRI

0

 Wanawake wawili wameuawa kwa kukatwa mapanga wilayani Nyang’wale mkoani Geita huku mmoja wao akiondolewa sehemu za siri na wauaji kuondoka nazo.

Akizungumza na mwananchi kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Jamhuri Wiliam amesema tukio la kwanza limetokea Kijiji cha Nyabulanda alfajiri ya Januari 16 wakati mama huyo akiwa shambani kwake.


Mkuu huyo wa wilaya amemtaja aliyeuawa na sehemu za siri kuondolewa kuwa ni Bigile Mweshemi (53) na kusema chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni mgogoro wa kifamilia na imani za kishirikina.

“Aliondoka na kwenda shambani alfajiri kwa hiyo hao wakata mapanga walimvamia na kumkata na mbaya zaidi wakaondoka na sehemu za siri mambo mengine yanatisha ndugu zetu hawa wana mambo magumu sana,” amesema.


Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na hadi sasa watu watatu wanashikiliwa.


 “Mmoja anayeshukiwa ambaye ni ndugu wa karibu waliyekuwa na mgogoro wa shamba kwa sasa ametoweka na wanaendelea kumsaka huyu ndiye anaedaiwa kuwatuma wakata mapanga,” amesema William.

Tukio jingine ni kikongwe aliyetambulika kwa jina la Melesiana Shija (70) mkazi wa Kijiji cha Nyugwa aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na wauaji kutokomea.

Mmoja wa wananchi Serafine Richard amesema mshukiwa aliyetoroka anadaiwa kuondoka kwa mganga  wa kienyeji saa 10 alfajiri na baada ya hapo tukio hilo likatokea na hadi sasa hajulikani aliko.


TAZAMA VIDEO HII ,BOFYA SASA USIPITWE

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top