MWIZI WA BATA ANUSURIKA KIFO POLISI WAMUOKOA MIKONONI MWA WANANCHI

0

 Kijana aliyejulikana kwa jina Musa amenusurika kuuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika eneo la Tambukateli kata ya Ndembezi Mjini Shinyanga baada ya kukamatwa na bata anayedaiwa kumuiba katika mtaa huo huku mwenyewe akikiri kufanya matukio ya wizi katika eneo hilo.


Tukio hilo limetokea majira ya sita mchana  Januari 3,2023 ambapo wananchi wenye hasira wamemshambulia kijana huyo kabla ya askari polisi kufika eneo la tukio na kumuokoa kijana huyo.

Wakati hayo yanajiri mkazi wa eneo hilo ambaye hatukufanikiwa kupata jina lake naye anaugulia maumivu baada ya kupewa kichapo wakati akizuiwa asimpige mtuhumiwa huyo wa wizi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top