MZEE AKATWA KOOO LAKE KISHA KUPORWA PESA AKITOKA BENKI

0

Mzee wa miaka 90 kutoka Kibwezi, Kaunti ya Makueni siku ya Jumanne, Januari 10,2023 aliuawa kinyama na majambazi.


mzee huyo alivamiwa na watu wasiojulikana alipotoka kwenye benki katika eneo la Metava kuchukua pesa zake alizopokea za mpango wa Inua Jamii.

Chifu wa eneo hilo Nicolas Mwonga alithibitisha kisa hicho, akisema majambazi hao walimkata koo mzee huyo na kumuibia pesa zake.

Mwili wa mwendazake umepelekewa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwenye Hospitali ya Kambu.

Polisi wameanzisha msako wa kuwanasa washukiwa ambao hadi sasa hawajakamatwa.

Hivi majuzi, Wizara ya Leba ilianza kupeana pesa za mpango wa Inua Jamii, baada ya kusubiri kwa miezi kadhaa. Chini ya mpango huo, yatima, wazee, na wanaoishi na ulemavu hupewa KSh 2000 (38,000tsh) kila mwezi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top