NABII MBARONI KWA TUHUMA ZA KUBAKA

0

 

Jeshi la polisi nchini Uganda limesema limemkamata Nabii na maafisa watatu wa polisi kufuatia kisa cha mwanamke mmoja raia wa kigeni kudaiwa kubakwa na kutapeliwa pesa zake.


Kukamatwa kwa Nabii huyo kunakuja baada ya kituo cha NTV-Uganda wikendi iliyopita kufanya mahojiano na mwathiriwa.


Katika mahojiano hayo, mwathiriwa kwa jina linahifadhiwa alifichua uyahawani ambao alitendewa na nabii Joseph Collins Twahirwa muda mfupi baada ya kuwasili nchini Uganda mnamo Disemba 11, 2022. Twahirwa alikuwa amemwalika mgeni huyo kwenda nchini Uganda kwa likizo.


Punde alipowasili nyumbani kwa nabii huyo, inasemekana alimpokonya pasipoti yake na kumwibia KSh37,203 na €400 sawa na (KSh53,698) kabla ya kumbaka. 

Raia huyo wa Latvia mwenye umri wa miaka 36, alisema Twahirwa alimwambia alitaka kupata mtoto na kisha alimsukuma kitandani na kumbaka usiku wa Disemba 11, 2022.


Inaelezwa kuwa mhanga baada ya unyama huo wa Nabii huyo alienda kuripoti katika Kituo cha Polisi cha Jinja Road na, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID) na alipofika hapo maafisa walimtaka mtalii huyo awanunulie mafuta ya gari lao au ashiriki ngono nao.


Mhanga huyo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alipokonywa simu yake na mawasiliano yote aliyokuwa nayo na Twahirwa kwenye mitandao ya kijamii yalifutwa ili kuharibu ushahidi wa uhusiano wao.


Hata hivyo mhanga huyo aliishia kuweka rumande kabla ya kuachiwa na kuonywa kukaa mbali na nabii huyo kwani anaushawishi na ana mahusiano na vigogo katika jeshi la Polisi.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa CID amesema kuwa maafisa hao watatu walikamatwa Jumapili, na Nabii huyo wa Epikaizo Ministries International yuko chini ya ulinzi wa Jeshi wakati shitaka lake likifikishwa mahakani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.


Polisi pia walitoa wito kwa waathiriwa wa Nabii huyo pia kujitokeza na kuwasilisha ripoti kwa CID ili kusaidia katika uchunguzi zaidi. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top