PAKA WA AJABU AMNG'ANG'ANIA MTOTO NA KUMG'ATA USONI

0

Joyce Japhet (5) mtoto mkazi wa kitongoji cha Kilimahewa kata ya Lulembela, wilayani Mbogwe mkoani Geita amenusurika kufa baada ya kushambuliwa na Paka ambae alimng'ata na kumng'ang'ania usoni  mpaka alipokatwa shingo ndipo akamuachia.


Paka huyo anayehusishwa na imani za kishirikina kabla ya kumshambulia mtoto huyo aliwashambulia pia watu wazima wanne katika eneo hilo kwa nyakati tofauti

"Nilisikia mtoto analia nimeumwa na Paka, baada ya kutoka pale akaja nae mpaka ndani yule mtoto amemshikilia sehemu ya shavu nikaona hivi na mimi nikajitahidi kuinyonga Ile paka, ikashindikana mpaka nikatumia kitu kikali yule paka kuchinja", alisema Marco Jopola jirani wa familia ya mtoto huyo

"Asubuhi Ile saa12 natoka nje kuchukua kuni Ile kugeuka hatua mbili nikasikia narukiwa na kitu, najitahidi kupambana nae ndio nikamrusha akawa amenichubua akakimbia baada ya muda wa saa3 nikasikia amemjeruhi mtoto mwingine", alisema Venance Mgula

Mwenyekiti wa kitongoji hicho Katendele Katendele amekiri kutokea kwa matukio ya watu watano kuvamiwa na Paka huyo ambaye baada ya kuchinjwa walimzika na baadae wakamkuta anapumua ndipo wakafikia maamuzi ya kumchoma moto.

"Nilikuta tayari washamzika yule paka na maamuzi waliyoyatoa baada ya kumfukua yule paka akaonekana kwamba anaguna walitoa maamuzi kwenda kumchoma walimpiga moto wakamchoma, lakini upande wangu nilielezea kwamba habari hizi jamani msiwe na hofu sana kwa sababu haya uwaga yapo, huwaga yanajitokeza lakini msifikiri kwamba ni uchawi, mapaka huwaga yanaingiliwa na kichaa kama mbwa", alisema Katendele.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top