MAZISHI YAAHIRISHWA BAADA YA WANAWAKE 3 KUGOMBANIA MWILI WA MAREHEMU

0

 

Shughuli za mazishi katika eneo bunge la Webuye kaunti ya Bungoma ziligoma kuendelea baada ya wanawake watatu ambao wote walikuwa wameolewa na mwanamume marehemu, kila mmoja kudai haki ya kuzika mwili wa mume wao.

Kulingana na ripoti iliyorushwa na runinga ya Citizen, wake hao watatu walianzisha zogo la kulaumiana kuhusu matukio yaliyojiri kabla ya mazishi yake, kila mmoja akisema alikuwa wa mwisho kutumia dakika za marehemu za mwisho naye.

Wazee katika kijiji hicho waliwataka wanawake hao wote kusuluhisha tofauti zao kabla ya mzee kuzikwa ili kukwepa mikosi ambayo huenda ikawaandama, kwani ni kinyume cha mila na tamaduni kwa jeneza kurudishwa nyumbani bila mwili, hivyo jeneza hilo haliwezi kutumiwa kumzika mzee.

“Na sisi kwa kimila ya Waluhya au Wabukusu, huwezi leta jeneza kwa boma bila mwili. Sasa hilo jeneza litarudi huko na halitatumika wakati kesi itakapokuwa imeisha,” alisema mzee mmoja.

Inaarifiwa kuwa mke wa tatu alimtuhumu mke wa kwanza kwa  kumtaka kukaa mbali na mazishi kwa kile alisema kuwa hakuwahi mhudumia kipindi anaugua.

Kwa mujibu wa tamaduni za Waluhya kutoka kaunti hiyo ya Bungoma, itabidi mwili wa mzee huyo ukarudishwa na jeneza jingine kununuliwa baada ya kuonekana wake hao watatu kila mmoja alitaka kupewa haki ya kumzika mzee.

Mke mmoja ambaye alizungumza na runinga hiyo alisema kuwa yeye hakuwa na shida yoyote kwani alitaka kumpumzisha mzee wake akisema kuwa aling’ang’ana naye hospitalini hadi akafia mikononi mwake.

“Mimi sina shida, wakiamua kuzika mzee, wacha mzee azikwe hatutaki vita, tunataka kuzika mzee wetu kwa amani kwa maana alikuwa mtu wa furaha. Haijalishi alikufa kwa mikono yangu kwa sababu nilishughulika na yeye mpaka dakika ya mwisho.”
BOFYA HAPA KUTAZAMA VIDEO HII
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top