TAARIFA MPYA KUTOKA CHADEMA SIKU YA KUZINDUA MIKUTANO YA HADHARA

0

 Kamati Kuu ya CHADEMA iliyokutana jana katika kikao chake cha dharura imetangaza kuwa uzinduzi rasmi wa mikutano yake ya hadhara kitaifa utafanyika tarehe 21 January 2023 na utafuatiwa na uzinduzi wa mikutano ya hadhara kila Makao Makuu ya Kanda na baadaye ngazi nyingine za Chama zitaendelea na mikutano kwenye ngazi zao.


Kwenye kikao hicho pia CHADEMA ilipokea na kujadili taarifa ya mwenendo wa mazunqumzo ya maridhiano baina ya Timu ya CHADEMA inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe na lle ya CCM/Serikali inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti Abdulrahman Kinana.

Taarifa iliyotolewa na CHADEMA leo imesema yafuatayo ------ “Baada ya kupokea taarifa hiyo na kujadili mwenendo wa mazungumzo na hatua ambayo imefikiwa mpaka sasa, Kamati Kuu kwa pamoja imeridhishwa na mwenendo wa mazungumzo hayo na hatua ambazo zimechukuliwa mpaka sasa na kuitaka Timu ya mazungumzo iendelee na mazungumzo ya maridhiano, Kamati Kuu imeagiza ngazi zote za Chama kuendelea na maandalizi ya kuanza kwa mikutano ya hadhara”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top