'TAMWA-ZNZ' YAWATAKA WAANDISHI WA HABARI KUZIPIGIA DEBE SHERIA ZA MAKOSA YA UDHALILISHAJI ZENYE KASORO ILI ZIFANYIWE MAREKEBISHO.

Hassan Msellem
0
Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba, wametakiwa kuzifanyia uchechemuzi Sheria za udhalilishaji zenye kasoro kufanyiwa marekebisho ili kuongeza mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji Nchini.



Kauli hiyo imetolewa na mratibu wa chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania 'TAMWA' Kisiwani Pemba Fat-hiya Mussa Said, katika mafunzo ya siku mbili ya kujadili vikwazo vinavyokwamisha ushiriki na ushirikishwaji wa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika harakati za kisiasa na kiuchumi katika ofisi za chama hicho Mkanjuni Chake Chake Pemba, amesema uwepo wa Shehia za udhalilishaji zenye kasoro ni miongoni mwa sababu zinazopelekea changamoto katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji Zanzibar.


"Ndugu wanahabari kwakweli Kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili katika kupambana na vitendo vya udhalilishaji lakini miongoni mwa changamoto hizo ni uwepo wa sheria ambazo sio rafiki, hivyo basi ni jukumu letu kuhakikisha tunazifahamu sheria hizo na kuzipigia debe ziweze kurekebisha ili kufanikisha mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji Zanzibar"

Akiwasilisha mada kuhusu kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika sheria za udhalilishaji mwendesha mashtaka kutoka Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Zanzibar, Ali Amour Makame, amesema sheria hizo ni pamoja na sheria nambari 6 ya mwaka 2018 ambayo inatoa adhabu ya kifungo pamoja na fidia kuwa sheria hiyo haikuweka wazi ni Kwa namna gani mshitakiwa anaweza kulipa fidia akiwa Chuo cha mafunzo, jambo ambalo linapelekea wahanga wa vitendo vya udhalilishaji kukosa fidia hizo.


"Ukiangalia Sheria hii utagundua kuwa kuna kasoro au mapungufu kwenye upande wa hukumu Kwa mfano unaweza kukuta kosa la aina moja lakini mmoja akahukumiwa Miaka 14 na mwengine akahukumiwa Miaka 30, suala hili linazusha maswali mengi Kwa wananchi lakini hata kwetu sisi waendesha mashtaka, hivyo sheria kama hii inapaswa kufanyiwa marekebisho ili kama ni kosa ni la aina moja basi na adhabu pia iwe Moja ili kuepusha dhana tofauti miongoni mwetu" mwendesha mashtaka Ali Amour Makame 

Aidha katika kipengele chengine ambacho mwendesha mashtaka huyo amesema kimeonekana na mapungufu ni kukosekana Kwa fedha za fidia Kwa familia ya muhanga kwani fidia hizo hazina muongozo nzuri wa walalamikaji kupata fidia hizo.


"Suala la fidia kwa familia ya walalamikaji bado hakujawa na utaratibu nzuri wa walalamikaji kupatiwa haki yao hiyo maana ni Kweli kwamba mahakama inamtaka mshitakiwa baadae ya kutiwa hatiani kutumikia miaka fulani pamoja na kumlipa mlalamikaji kiasi fulani cha fedha lakini tangu nianze kazi hii sijawahi kuona fidia hizo zikitoka Kwa mshitakiwa kwenda familia za walalamikaji, sasa hapa napo panaonekana Pana shida kubwa kuanzia upande wa mahakama pamoja na wananchi" alisema

Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar Leo na blog ya Pembatoday Haji Nassor Mohammed, amesema changamoto nyengine inayopelea familia za walalamikaji kukosa haki yao ya fidia ni pamoja na kutokufahamu taratibu za kisheria katika kudai haki yao hiyo.


"Mimi nadhani licha mahakama kutokuwa na utaratibu nzuri wa kuhakikisha kuwa walalamikaji wanapatiwa haki yao ya fidia lakini na wananchi wenyewe nao hawajui nini wafanye endapo wanahisi ni muda mrefu sasa hawajapitwa fidia, ambapo jambo ambalo walipaswa kufanya ni kufungua kesi ya madai" alishauri


Inaendelea................

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top