UKATILI ELIZA AUAWA USIKU KISHA MWILI WAKE KUTUPWA

0

 

Eliza Mlimbila (17) mhitimu wa kidato cha Nne 2022, mkazi wa Sigridi Makambako Njombe ameuawa na watu wasiojulikana siku ya mkesha wa mwaka mpya na mwili wake kutupwa mtaa wa Kahawa huku ukiwa na Majeraha.


Akisimulia mkasa huo baba mzazi wa Marehemu aitwaye Meshack Mlimbila amesema kuwa Desemba 31 mwanaye alichelewa kurudi nyumbani na baada ya kumuuliza kwanini amechelewa ndipo Marehemu alipoondoka na kutokomea pasipojulikana.


“Siku ya Ijumaa aliondoka alirudi usiku na Jumamosi sisi wakati tunatoka shambani hatukumkuta mpaka saa tatu usiku nilipomuuliza na alipoondoka ondoka sikuelewa kabisa na kwa kua imekuwa ni kawaida kuondoka na kutokurudi nikajua atarudi ila ndo nakuja kusikia ameokotwa Kahawa akiwa amekufa na mara kadhaa tumejaribu kumkanya lakini amekuwa akiendelea na magenge”

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Selemani Issah amehudhuria ibada ya mazishi ya binti huyo na kusema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuwakamata wale wote waliohusika kutekeleza mauaji hayo.


Mbunge wa jimbo la Makambako na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ni miongoni mwa walioshiriki maziko hayo ambaye amelaani vikali kitendo hicho cha ukatili.


Kwa mujibu wa Taarifa za baadhi ya Ndugu wa Eliza akiwemo mjomba wake ni kuwa mwili wa Eliza ulionyesha kubakwa na kulawitiwa huku Salama Mwabena jirani wa Marehemu akieleza kuwa Kabla ya umauti kumkuta Eliza alipita nyumbani kwake majira ya saa tatu usiku akiwa na kibegi mgongoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top