VIONGOZI WA CCM WASHAMBULIWA NA MORANI WA KIMASAI ARUSHA

0

Viongozi nane wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Engaruka wilayani Monduli, mkoani Arusha, wamepigwa na kujeruhiwa sehemu Mbalimbali za Miili Yao na kundi la wananchi wakati wakifuatilia migogoro ya ardhi.



Viongozi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru wameeleza kuwa wananchi hao wa Kijiji cha Engaruka wakitumia Silaha za jadi kama Sime, Mikuki na Marungu, waliwashambulia kwa madai ya hasira za kuuzwa kwa ardhi ya kijiji hicho kinyemela.

Tukio hilo limetokea Januari 10, 2023 wakati viongozi hao ambao ni wajumbe wa kamati ya siasa ya chama hicho walipokwenda kijijini hapo kufuatilia tuhuma za Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abrahamu Logolie kudaiwa kuuza ardhi kinyemela.

Majeruhi hao wanaeleza kuwa mara baada ya kufika katika kijiji hicho kilichopo takriban kilomita 60 kutoka Monduli Mjini, walivamiwa na kushambukiwa na kundi la vijana wa kimasai maarufu kama Morani zaidi ya 30 waliokuwa wamejikusanya.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Frank Mwaisumbe akizunguzmia tukio Hilo amesema miongoni mwa viongozi walioshambuliwa ni Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo, Leliya Sengeita, Katibu wake, Joseph Namoyo ambao wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.

Mwaisumbe amesema uchunguzi Wa Tukio Hilo unaendelea huku Vyombo Vya ulinzi na Usalama vikimshikilia mwenyekiti wa kijiji hicho, Abrahamu Logolie ambaye inadaiwa alishirikiana na viongozi wengine wa Serikali ya Kijiji kuandaa mpango huo wa vijana kuwashambulia viongozi hao wa chama.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top