WATOTO WIWILI WAFA BAADA YA KUDUMBUKIA KWENYE DIBWI LA MAJI

0

Watoto wawili wakazi wa mtaa wa Nyantorotoro B Mjini Geita wanaofahamika kwa majina ya Jebras Maiko ( 3 ) na Mariamu lameck (mwaka wa mmoja na nusu) wamefariki dunia baada ya kudumbukia kwenye dimbwi la Maji lillilopo jirani na nyumbani.

PICHA KUTOKA MAKTABA

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa wa Jeshi la Uokoaji na Zimamoto mkoa wa Geita, Emmanuel Ndoshi amesema awali watoto hao walienda bwawani hapo na mama yao na na waliporudi nyumbani walirejea tena peke yao.

"Tumetoa wito kwa serikali ya mtaa huu kuwa maeneo haya hayana budi kuwekewa ishara ya hatari, yaani pawe na kiashiria.”

Mwenyekiti wa mtaa wa Nyantorotoro B, Makwendera Magwehoroka amesema taarifa ya tukio aliipata muda wa saa mbili usiku na walifika eneo la tukio na kukuta watoto wameshafariki na wameshatolewa.

"Ni tukio la kuhuzunisha kwa kweli maana walikuwa watoto wadogo kabisa."

"Wazazi muangalie watoto zenu kwa uangalifu mkubwa sana maana haya maeneo ya mtaani, na kuna mashimo mengi hatari hasa kipindi hiki ni cha mvua.” Amesisitiza Mwenyekiti wa Mtaa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top