'ZAFAYCO' YATOA ELIMU YA UTAWALA BORA KWA VIJANA 160 KISIWANI PEMBA.

Hassan Msellem
0

Vijana Kisiwani Pemba wametakiwa kufuata misingi ya Uadilifu na Uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao.


Hayo yamesemwa na Ndugu Bakari Omar Ali kutoka Idara ya katiba na msaada wa kisheria katika mafunzo ya utawala bora yaliyotolewa kwa vijana 40 kutoka Wilaya ya Chake Chake, amesema endapo vijana watafanya shughuli zao kwa misingi ya uadilifu na uwajibikaji wataweza kunufaika kwa kiasi kikubwa wao na Taifa kwa ujumla.


Aidha, amewataka vijana hao kutokujiingiza katika vitendo vinavyoweza kukatisha ndoto zao ikiwemo mahusiano yasiyo salama, wizi pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa jumuiya ya kupambana na changamoto za Vijana (ZAFAYCO) Abdalla Ali Abeid, amesema jumuiya hiyo imewafikia vijana 17311 Zanzibar kutoka mwaka 2011 hadi mwaka 2022 idadi ambayo imeleta mabadiliko chanya kwa vijana.


Ameongeza kuwa, jukumu la kutoa elimu juu ya vijana Kujitambua, Afya ya Uzazi pamoja na Utawala ni bora ni jukumu la kila taasi kwani vijana wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ufanyaji wa ngono zembe pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya.


Nao Vijana hao wameipongeza jumuiya hiyo (ZAFAYCO) kutokana Mafunzo hayo ya Utawala bora nakuahidi kuyafanyia kazi ipaswavyo ili yaweze kuwaletea maendeleo.


Mafunzo hayo yametolewa na jumuiya ya kupambana na changamoto za vijana (ZAFAYCO) kwa kushirikiana Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala bora ambapo jumla ya vijana 160 wamefikiwa Kisiwani Pemba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top