AVAMIA KANISA KATOLIKI GEITA, AHARIBU VITU VITAKATIFU

0

 

Sehemu ya uharibifu uliofanywa


MTU asiyefahamika amevamia na kuingia ndani ya kanisa Katoliki jimbo la Geita na kufanya uharibifu katika altare na sakrestia na kuvunja tabernakulo, kumwaga ekaristi takatifu na kuchana kitabu kitakatifu Biblia sambamba na kuharibu mfumo wa camera za ulinzi.

Taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Geita kwa njia ya simu Flavian Matindi Kasalla amesema mtu huyo alivunja kioo cha mlangoni na kuharibu madhabahu takatifu huku akiharibu sehemu mbalimbali za ibada na kuharibu vitabu vitakatifu.
“Mpaka sasa hatujajua alikotokea na wala hatujui aliingia saa ngapi japo ilikuwa ni usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, kanisa letu linalindwa na kampuni ya ulinzi ila mpaka sasa ni kitendawili kuwa mlinzi alikuwa wapi.

Mtu aliyefanya tukio hilo amekamatwa na ameshafikishwa katika vyombo vya usalama pamoja na mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo” amesema Askofu Kasalla.
Watu wawili wanashilikiwa na jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.

 Akithibithisha kukamatwa kwa watu hao, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlay amesema jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini nani kamtuma na sababu za kufanya uharibifu huo.
“Mtu huyo anaonekana alikuwa mlinzi na ni mtu ambaye amekuwa akihudumu katika kanisani haswa huko alikotoka Bukoba hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na itakapobainika tutatoa taarifa zaidi kwani mpaka sasa kuna mambo tunayafuatilia tatutayazungumza ili kutovuruga upelelezi.

BOFYA KUTAZAMA VIDEO HII
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top