Watoto ni baraka kutoka kwa Mungu, na watu wengi wanaamini kwamba ni Mwenyezi Mungu pekee ndiye mwenye kauli ya mwisho kuhusu ni wana wangapi atampa mja maishani mwake.
Ingawa wengi wanaweza kupendelea mtoto mmoja kwanza, uwezekano wa kujifungua pacha, au watoto zaidi kwa mpigo upo kila wakati na inaweza kuleta mkanganyiko katika familia changa ikiwa haijatayarishwa kwa jukumu kama hilo.
Mwanamke alifahamika kwa jina la Wangar kutoka nchini Kenya ameonyesha wasiwasi wake baada ya kujifungua pacha kwa mpigo huku penzi lake na mumewe likiingia doa.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 25 alisema matatizo yalizuka baada ya kujifungua pacha hao mwaka wa 2020 ndipo Mumewe alipomkimbia.
Mama huyo wa Nakuru alihuzunika moyo kwani mpenzi wake wa roho alimwacha alipomhitaji zaidi kulea watoto na kwamba kuzaa pacha kunachukuliwa kuwa laana katika jamii yake.
Alikiri haikuwa rahisi kutunza watoto kwani alihitaji msaada wa mahitaji ambayo yalikuja na malaika hao. Mama huyo mwenye bidii alifichua kwamba analazimika kuwabeba watoto kwenye toroli anapofanya kazi za vibarua kuwalisha.
ULITAZAMA VIDEO HII YA WANAWAKE WALIOGANDA BARABARANI?