MAHAKAMA ya Wilaya Mpanda mkoani Katavi, imemuhukumu Agustino Michese (59) kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka bintiye mwenye umri wa miaka 16.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Mpanda Rebeka Mwalusako, amesema wakati akisoma hukumu hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe tofauti za mwezi Mei hadi Disemba 30, 2022 katika kijiji cha Isinde.
Kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 158 kifungu kidogo cha (1) (a) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyo fanyiwa marejeo mwaka 2019.
Hata hivyo mtuhumiwa wakati akisomewa maelekezo ya awali amekili kutenda kosa hilo huku akijitetea kuwa alikuwa amelewa hivyo alijua anaefanyanae tendo hilo ni mke wake.
Upande wa mashitaka umeleta mashahidi watano akiwemo mtoto mwenyewe ambapo mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa wakati akitoa ushahidi wake alisema baba yake amemfanyia kitendo hicho mara tatu huku akimtaka kutopiga kelele endapo atapiga atamfanyia kitu kibaya.
HILI HAPA TAMKO LA SERIKALI KUHUSU DIGRII ZA KUNUNUA WABUNGE