Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo wahakikishe wanamfikisha katika vyombo vya sheria baba mzazi wa mwanafunzi wa darasa la pili (7) katika Kata ya Sokoni One mtaa wa Lonovono Jijini Arusha kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake.
Waziri Mkuu amesema Serikali inakemea vikali vitendo vya unyanyasaji, ubakaji na ulawiti kwa watoto, hivyo imewataka Wakuu wa mikoa na makamanda wa polisi nchini wahakikishe wanawasaka na kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu.
Ametoa agizo hilo l Februari 17, 2023 baada ya kusambaa kwa taarifa kupitia vyombo vya habari vikimuonesha mtoto huyo ambaye anadaiwa kulawitiwa na baba yake mzazi. Mtoto huyo ambaye alisikika akielezea namna mzazi wake huyo alivyokuwa akimfanyia vitendo vya ukatili naye atafutwe na kupatiwa huduma ya matibabu kwa haraka.
TAZAMA VIDEO HII KUHUSU FEI TOTO