BINTI ATAKIWA KULIPA FIDIA MPENZIWE KWA KUKATAA KUOLEWA NAE

0

 Mahakama nchini Uganda imemuamuru mwanamke wa Wilaya ya Kanungu amlipe mchumba wake USh 10 milioni (Sawa na Mil. 6,375,985 za Kitanzania) kama fidia kwa kukataa kuolewa naye.


Kwa mujibu wa stakabadhi za mahakama Tumwine na Fortunate Kyarikunda walipendana 2015 na kisha kuingia katika ahadi ya kuoana 2018. 

Tumwine anayefundisha katika Shule ya Msingi Kiringa, aliiambia mahakama kuwa alimsaidia Kyarikunda kifedha pamoja na kumfadhili kusomea kozi ya stashahada ya sheria katika Kituo cha Maendeleo ya Sheria (LDC). Aliambia mahakama kuwa alitumia zaidi ya Sh milioni 9.4.

Kwa mujibu wa Hakimu Asanasio Mukobi ahadi ya kuoana haikutimizwa na Kyarikunda na kwa hivyo, ilikuwa na madhara kwa mpenzi wake. 

Hilo ndilo lililomfanya awe na haki ya kurejeshewa fedha alizotumia kumfadhili.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top