KIBOKO AMJERUHI MWANANCHI NAE AMKATA MKIA

0

Mtu mmoja amejeruhiwa kwa kuvunjwa mguu sehemu ya paja na mnyama kiboko juzi usiku akiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Mngoji mkoani Mtwara na daktari amedhibitisha kuwa mtu huyo alifika na kupatiwa matibabu.


Akizungumza na Mwananchi Digital, Ginasio Francis (aliyeumizwa na kiboko) mkazi wa Kijiji cha Mngoji, Kata ya Madimba alisema kuwa alijeruhiwa usiku akiwa nyumbani kwake.

“Nilikuwa nimelala juzi saa 4 usiku nilisikia kitu kinatembea nje ya nyumba yangu nilifungua mlango nikamuona mnyama kiboko. Nikarudi ndani kufuata silaha, kitendo cha kuwasha taa, kiboko akaona mwanga akajificha,” amesimulia.


“Nilipotoka nje sikumuona kumbe amejificha chini ya mkorosho wakati namtafuta kumbe yuko nyuma yangu akanibeba, akanikimbiza kwa umbali Fulani kisha akanitupa. Aliponitupa, nilikuwa bado nimeshika panga hivyo nikamkata mkia, hapo ndio nilimtia hasira, tukaanza kupambana. Alivunja mguu wangu mifupa yote imekuwa unga.”

Somoe Namurunga ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Mngoji, alisema kitendo cha mtu huyo kupata majeraha katika kijiji hicho kimeongeza hofu zaidi.


“Tunaishi kwa mashaka hata kwenda shamba tunaogopa na sisi maisha yetu ni maporini hatuna amani kabisa. Mtu kujeruhiwa inatia mashaka sana, tunaomba serikali itusaidie ili tuweze kuishi kwa amani hatuna, watuondolee huyu mnyama,” amesema Namurunga.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Ligula, Zawadi Bwanali alisema kuwa mgonjwa huyo alipokewa na kupatiwa matibabu kisha kupewa rufaa ili aweze kupata matibabu ya kibingwa zaidi.

“Tumepokea mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Francis aliyejeruhiwa na mnyama kiboko alifika akiwa na fahamu, tulimhudumia mguu ambao ulikatika mara mbili na kusagika ambapo alikuwa na upungufu wa damu ambayo nayo pia aliongezewa na anaendelea na matibabu,” alisema Bwanali.


“Mgonjwa ameumia kwenye paja sehemu mbili juu na chini ambapo mfupa ulitoka na tumesha mhudumia na anaendelea na matibabu na tumempeleka kwenda kupata huduma za kibingwa zaidi,” alisema Bwanali.


TAZAMA VIDEO HII MPAKA TAMANI

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top