KIJANA ADAIWA KUUAWA KWA KUPIGWA BAR WAKINYWA ULABU NJOMBE

0

 Kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24 Claudia Mbogela amekutwa amefariki dunia kwenye mazingira ya baa iliyopo Kijiji cha Iniho Wilayani Makete Mkoani Njombe.

Picha kutoka Maktaba


Tukio hilo limetokea jana Februari 12, 2023 ambapo imeelezwa marehemu inadaiwa alipigwa na kitu butu katika sehemu mbalimbali za mwili wake.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Iniho Rabson Luvanda akizungumza na kituo cha redio Kitulo FM amesema walipata taarifa kutoka Kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya mabasi ambaye anakatisha tiketi Kijijini hapo na walipofika eneo la tukio wakakuta mwili wa kijana huyo.

Baada ya uchunguzi wa Dadaktari imeelezwa kwamba kijana huyo alipigwa na kitu butu kwenye maeneo mbalimbali ya mwili mpaka kupelekea kupoteza uhai wake.

Akieleza zaidi Mwenyekiti huyo amesema chanzo cha tukio hilo inadaiwa kuwa ni ugomvi ulioibuka kati ya kijana huyo aliyefariki na vijana wengine waliokuwa wanakunywa pombe kwenye Baa hiyo huku vijana hao ambao hawakutambulika mara moja wakitoweka baada ya kutenda kosa hilo na walifika kijijini hapo kwa ajili ya kufanya kazi ya kupasua mbao.

Chanzo:Kitulo FM
USIPITE BILA KUTAZAMA VIDEO HII
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top