Mtu moja aliyetambulika kwa jina la Musa Robert anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 76 mkazi wa Kijiji cha Kasheka kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza amekutwa amefariki dunia pembezoni mwa ziwa Victoria katika kitongoji cha Kisenya Kijiji cha Katwe kata ya Katwe wilayani humo huku sehemu zake za siri zikiwa zimenyofolewa.Picha kutoka Maktaba
Ofisa mtendaji Kijiji cha Katwe, Ezekiery Galula akizungumuza na Mwananchi February 12, 2023 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeleta simanzi kwa wananchi wa maeneo hayo.
Amesema alipata taarifa kutoka la raia wema waliopita maeneo hayo wakiwa wanakwenda kufanya shughuli za kujipatia kipato ndipo walipoona mwili huo na kutoa taarifa.
Mdogo wa marehemu Manyindo Robert (74) amesema kaka yake alikuwa anatoka nyumbani kwao Kijiji cha Kasheka kwenda Kijiji cha Katwe Kitongoji cha Kisenya kusalimia ndugu na jamaa alipokaribia maeneo hayo alisikia wananchi wakipiga yowe kama ilivyo mila na desturi aliungana na wananchi wa maeneo hayo hadi sehemu ya tukio na alipofika alimutambua kuwa aliyefariki kuwa na kaka yake.
Manyindo amesema sehemu za siri kwenye mwili wa marehumu kaka yake zilikuwa zimenyofolewa na hazijulikani zilipo licha na viungo vingine kuwepo.
"Kitu kilichonitambulisha ni vidole vyake, kichwa sambamba na nundu aliyokuwa nayo mgongoni, kilichoondoa uhai wake hata mimi sikuelewi mwili huu umesafirisha hadi nyumbani kwake Kijiji cha Kasheka kwa ajili ya maziko, marehemu ameacha mke na watoto wanane.” amesema Manyindo.
Endelea kusoma zaidi <BOFYA HAPA>
HEBU SIKIA KAULI HII YA SERIKALI ISIKUPITE