MCHUNGAJI AGHUSHI KIFO KUKWEPA KULIPA DENI LA MUUMINI WAKE

0

Mchungaji mmoja Mnigeria anadaiwa kughushi kifo chake na kuchapisha habari za kufariki kwake mitandaoni katika jitihada za kukwepa kulipa deni la zaidi ya KSh819 alizokopa kutoka kwa muumini wa kanisa lake. 

Pasta huyo aliyetambuliwa kwa jina Paul Oyewole, alichapisha habari za kifo chake kwenye mtandao wa Whatsapp baada ya kutuma ujumbe feki wa pesa kwa mkopeshaji wake Boyede Emmanuel ilhali hakuwa na pesa hizo kwenye kaunti ya benki yake.

Oyele alifikishwa kortini kwa kosa la kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu akisingizia kurudisha fedha hizo ndani ya siku saba. 

Mtumishi huyo wa Mungu pia alidaiwa kumtisha Emmanuel, akisema atavua nguo zote mbele ya nyumba ya mlalamishi. 

Inasemekana kuwa alitenda kitendo hicho kati ya Novemba 2021 na Mei 2022 Hata hivyo, alipofikishwa mahakamani, Oyewole, mwenye umri wa miaka 43, alikana mashtaka hayo dhidi yake huku mwendesha mashtaka Sajenti Akao Moremi akisema atawashirikisha mashahidi wanne kutoa ushahidi katika kesi hiyo. 

Wakili wake, Queen Arokoyo, baadaye aliomba mteja wake aachiliwe kwa dhamana ambapo korti ilimwachilia mshtakiwa kwa dhamana na kesi hiyo ikaahirishwa hadi Februari 13.2023 ambapo itasikilizwa tena.

KAMA HUJATAZAMA VIDEO HII TAZAMA SASA

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top