Watoto wawili wa familia moja wakazi wa Kitela, mji mdogo wa Makongorosi, Chunya mkoani Mbeya, wamefariki dunia huku watatu wakinusurika baada ya kunywa dawa waliyopewa na mganga wa kienyeji kwa madai ya kutibiwa tumbo kutokana na familia hiyo kusumbuliwa na maradhi ya tumbo mara kwa mara.
Mkuu wa wilaya ya Chunya Mayeka Saimoni Mayeka, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema familia hiyo ilikunywa dawa hiyo pamoja na mama yao mzazi aliyejulikana kwa jina la Dukila Msangisa na kuanza kutapika na kuharisha kabla ya kupelekwa zahanati ya Mwananchi iliyopo Makongorosi ambapo walipatiwa huduma ya kwanza na kupewa rufaa hospitali ya wilaya Chunya, ambapo wakiwa njiani vijana hao wawili walifariki na miili yao kuhifadhiwa hospitali ya wilaya.
Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya halmashauri ya ya Chunya Edward Tengulaga Mwakasungu, amethibitisha kupokea kupokea miili ya watoto wawili wa kiume, Njile Makelemo (26), na Mafunda makelemo (18).
Tengulaga amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali miili hiyo imefanyiwa uchunguzi kwa kuchukua sampuli ya ini,figo na tumbo ili kuona aina ya dawa iliyotumika mpaka kupelekea vifo hivyo.
Mkuu wa wilaya ya chunya Mayeka Saimoni Mayeka amesema tayari polisi inamsaka mganga huyo ambaye alitoroka mara baada ya kutokea kwa vifo hivyo na kuonya baadhi ya waganga wanaotoa tiba chonganishi
KAMA HUKUTAZAMA VIDEO HII BASI ISIKUPITE