MKE AMNG'TA BABA MKWE WAKE SEHEMU ZA SIRI

0

Polisi katika kaunti ya Bungoma  nchini Kenya wanachunguza kisa ambapo mwanamke mmoja anadaiwa kumng'ata baba mkwe wake sehemu za siri wakati wa ugomvi.


Katika kisa hicho cha kustaajabisha ambacho kimeshtua familia na majirani, Vincent Simiyu mwenye umri wa miaka 78, kutoka kijiji cha Kimaeti eneo bunge la Bumula, anauguza majeraha kufuatia kuumwa uume wake na mke wa mtoto wake.

Kulingana na mashahidi, mshukiwa Everline Okelo, anadaiwa kukasirishwa na baba mkwe wake baada ya kupata fununu kwamba alikuwa anafahamu mwanawe alioa mke wa pili.

Simiyu alisimulia kuwa Okelo alimpiga kwa jiwe na kuanguka chini na baadaye kumkalia kifuani huku akimshika uume wake alioweka mdomoni na kuuma.

Wazee wa Bukusu walisema mwanamke huyo ni lazima aadhibiwe kitamaduni kwa kuwa mila za jamii hiyo zinamzuia kukaribiana kimwili na wakwe zake.

Mtuhumiwa wa tukio hilo ametoweka mara baada ya kufanya jambo la kushangaza huku majeruhi akikimbizwa hospitali kwaajili ya kupatiwa matibabu.
TAZAMA VIDEO HII KWA KUBOFYA KATIKATI KUTAZAMA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top