Mwalimu Wa kujitolea katika shule ya sekondari Sinde jijini Mbeya, Evarist Chonya ameibua taharuki baada ya kuwakusanya wanafunzi wa shule hiyo na kuwapiga picha wakiwa wamekaa chini Kisha kuzisambaza katika mitandao ya kijamii.
Akielezea tukio hilo mkuu wa shule hiyo Anatalia Luhungo, amesema mwalimu huyo aliwakusanya wanafunzi wakiwa kwenye zoezi la kuandika majina katika madawati na kuwarejesha darasani Kisha kuwapiga picha wakiwa wamekaa chini huku madawati yakiwa nje.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Wakili Triphonia Kisiga amesema tayari wameanza kumchukulia hatua mwalimu huyo kwa kumfikisha katika vyombo vya Sheria kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo, Huku afisa elimu Mkoa wa Mbeya Mwl. Ernest Hinju akiwataka vijana walioaminiwa na shule kujitolea kufuata maelekezo wanayopewa na viongozi wao.