MWANAFUNZI MBARONI KWA KUMCHOMA KISU MWALIMU AKIFUNDISHA..AFARIKI DUNIA

0

 Mwalimu mmoja ameuawa mikononi mwa mwanafunzi wake ambaye alimshamubulia kwa kisu katikati ya somo. 

PICHA KUTOKA MAKTABA HAIHUSIANI NA TUKIO HALISI

Katika tukio hilo la Jumatano, Februari 22,2023 lililotokea magharibi mwa Ufaransa, mwalimu huyo wa Kihispania mwenye umri wa miaka 52, alikuwa akifundisha darasani wakati mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, alipomshambulia kwa kisu. 

Shirika la habari la AFP likinukuu ripoti ya gazeti la Sud Ouest, lilisema kuwa mvulana huyo aliingia darasani wakati wa somo la Kihispania la mwalimu huyo alifunga mlango wa darasa hilo kwa ndani na kumchoma kisu mwalimu kifuani mwake. 

Kisha mwalimu huyo wa kike alifanyiwa huduma ya kwanza lakini alifariki kutokana na majeraha aliyopata huku mwanafunzi huyo akikamatwa na kwa sasa anazuiliwa na polisi. 


Kufuatia tukio hilo katika Shule ya Saint-Thomas d'Aquin, wanafunzi wote walizuiliwa kwenye madarasa yao kwa takriban saa mbili kabla ya kuruhusiwa kuondoka taratibu. 

HII NDIO ILE VIDEO ILIYO TRENDI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top