RAIS SAMIA ATOA SIRI KUFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

0

Rais Samia Suluhu Hassan amesema alidhani jeshi lililokuwapo (Baraza la Mawaziri) angekwenda nalo mpaka mwisho wa muhula wake lakini ameeleza kuwa katika safari ajali hutokea.


Hiyo ni baada ya kufanya uteuzi wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na kumuacha aliyekuwa akishikilia kiti hicho Mashimba Ndaki kwa kumuweka Abdallah Ulega.

Ameyaeleza hayo leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma katika hafla ya kuwaapisha vuongozi aliowateua  Jumapili february 26 2023.


Rais Samia amesema katika mabadiliko hayo madogo amemdondosha Waziri mmoja pekee.

"Nilidhani kuwa lile jeshi lililopo tungekwenda nalo mpaka tuvuke ule mwamba wa kuingia upande wa pili, katika safari ajali zinatokea mwingine anajikwaa anaanguka.

Amemtaka Ulega aliyechukua nafasi ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuhakikisha ugomvi wake na wao utamalizwa kwa kufanya kazi na anataka kuona Mifugo na Uvuvi inanyanyuka.

"Nakuamini na nadhani utaweza, kama wakati ule ulikuwa hufanyi, kwa sababu ulikuwa chini ya mtu sasa utaonekana unafanya kwa sababu hauko chini ya mti au nawewe utakuwa kama wale, safari bado ni ndefu tuna miaka miwili mbele yetu, nikuombe ukafanye kazi.

Amesema mabadiliko hayo ni ya kwaida katika kuimarisha utendaji ndani ya Serikali, ndiyo maana mabadiliko makubwa yamefanyika katika ngazi ya makatibu wakuu lengo ikiwa ni kuweka nguvu moja ili kwenda na kasi inayohitajika.

"Tumejitahidi kunyofoa katika maeneo mliyopo kujaza nafasi hizo, tukijua kuwa kila mtu anaelewa eneo lake alilopo," amesema Rais Samia.

Amesema mabadiliko hayo pia yamevuta watu walio nje ya Serikali kwa malengo  kuwa watakuja na mawazo mapya na kuona ndani ya Serikali nini kinafanyika wakichanganya na wao mambo yatakwenda vizuri.

"Tutaendelea kunyofoa huko na kuleta ndani ili atusaidie Serikali kwa sababu akikaa nje kazi ni kulaumu tu, hajui ugumu uliomo ndani ya serikali, wakiingia tutafanya nao watupe uzoefu wao waone yaliyopo serikalini ili twende kwa pamoja,” amesisitiza.


Kuhusu Katibu Mkuu Uwekezaji ambaye waziri wake hakutajwa, amesema wamemtanguliza yeye ili asaidie kupanga yanayotakiwa kupangwa huku akieleza kuwa anataka maeneo matatu muhimu yarudi chini ya Ofisi ya Rais na baadaye michakato na sheria ikikamilika itakuwa wizara kamili.

"Kwa sasa tunaleta, Msajili wa Hazina, Tume ya Mipango na Uwekezaji zinakuja chini ya Rais. Tutakuwa na waziri wake na naibu waziri wake, tukimaliza mchakato wa sheria itakuwa wizara kamili.


 Kwa sasa tumetanguliza katibu mkuu atusaidie kupanga, tunafanyaje wanakaaje, mambo ya uchumi, uchumi mkubwa na mdogo tunafanyaje atusaidie kupanga.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top