SANGA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA TSH 500,000/=

0

 Mahakama ya Wilaya ya Mufindi imemhukumu mkazi wa Changarawe mjini Mafinga, Irene Sanga,(19) kulipa faini ya Sh500,000 au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuiba mtoto mwenye umri wa miaka minne.

Hukumu hiyo inetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Sekela Kyungu baada ya mshitakiwa kukiri kuiba mtoto huyo.

Sanga alikiri kuiba mtoto Januari 25, 2023 kinyume na kifungu namba 40 na 51(a) cha sheria ya Mtoto Sura 13 Rejeo la 2019

Kulingana na maelezo ya kosa hilo, Hakimu Kyungu amesema siku ya tukio, mshitakiwa wakati anatokea huko eneo la Changarawe alimkuta mtoto huyo barabarani na akamchukua na kwenda naye nyumbani kwake anakoishi.

Baada ya kumchukua, alikaa naye kwa siku tisa nyumbani lakini ilipofika siku ya sita, alimnyoa nywele na kumnunulia nguo zingine kwa lengo la kumbadilishia muonekano aliokuwa nao hapo awali ili watu wasiweze kumtambua.

Hata hivyo, baada ya kumnyoa nywele kwa staili ya kiduku, ilipofika siku ya tisa majirani waligundua binti hiyo anaishi na mtoto huyo, walimkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Mafinga taarifa zilipokuwa zimefunguliwa.

 USIPOTAZAMA VIDEO HII USIJE JILAUMU BAADAE KWA KUCHELEWA KUTAZAMA
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top