Wanafunzi 82 wa shule ya sekondari Lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe wamenusurika kuungua baada ya bweni lao kuteketea kwa moto na kuunguza mali za wanafunzi na za shule zenye thamani zaidi ya sh. milioni 18.
Akizungumza kuhusiana na tukio hilo mkuu wa shule hiyo Everine Somola, amesema kuwa,tukio hilo limetokea majira ya saa tatu wakati wanafunzi wakiwa kwenye masomo ya usiku.
“Bweni hili wanaishi wanafunzi 82 ambao ni wavulana na wakati moto unatokea hakukuwa na mwanafunzi bwenini kwani ilikuwa ni muda wa masomo ya usiku hivyo walikuwa darasani,” amesema.
TAZAMA VIDEO HII KUPATA TAARIFA KAMILI