Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amefika kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, RPC Martin Otieno akitaka kuliangalia gari lake ambalo anasema alishambuliwa akiwa nalo.
Lissu amefika Alhamisi, Februari 9, 2023, huku akisema kuwa alikuwa amewasiliana na RPC kwa ajili ya kwenda kuliona gari lake hilo ambalo hata hiivyo bado hajafanikiwa kuliona akielekezwa kurudi wakati mwingine.
Lissu ameeleza kuwa ameambiwa arejee baadaye ili aweze kuonana na RPC Otieno ili aweze kupata utaratibu wa kuliona gari lake, pamoja na kujua namna ambavyo anaweza kukabidhiwa.
SPIKA WA BUNGE ATAKA MANENO YA MWIGULU YAFUTWE