Wananchi wa Kisiwa cha Makoongwe Mkoa wa Kusini Pemba, wameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kuwasogezea kwa ukaribu huduma za kipolisi na mahakama ilikuepukana na usumbufu wanaokumbana nao wakati wakihitaji huduma hizo.
Wakizungumza kwenye mkutano maalum na watendaji wa mahakama
huko skuli ya Makoongwe, wamesema umbali wa upatikanaji wa huduma hizo unachangia
kwa kiasi kikubwa kutokupata haki zao kwa wakati sambamba na kukosekana kwa haki
hizo.
Alieleza mmoja wa wananchi “Waheshimiwa chanzo kikubwa kwa sisi
wananchi wa Makoongwe masafa makubwa ya upatikanaji wa huduma za Polisi na
Mahakama, kama munavyofahamu kuwa sisi tuko kwenye Kisiwa na huku hakuna hata
kituo kidogo cha Polisi kwahivyo mwananchi anapokuwa na kesi yake inambidi
mpaka avuuke mpaka Mkoani ndipo apate kituo cha Polisi na kuanza mchakato wa
kwenda mahakamani, kwahivyo tunawaomba sana kwa hili mutuangalie ili na sisi
tuapate angalau kituo kidogo cha Polisi ili tuweze kupeleka kesi zetu”
“Binafsi nilikuwa na
kesi ya mume wangu ya kunitelekeza na familia nilipambana sana ili kuhakikisha
napata haki yangu lakini kutokana umbali wa huku ninakoishi gharama zinakuwa ni
kumbwa mno na dana dana zilikuwa nyingi nikashindwa kuapata haki yangu hadi
niliposafiri kwenda Unguja ndipo nikafanikiwa” alisema mama huyu
Alieleza changamoto mbali mbali walizoziibua mara baada ua
kumalizika kwa mkutano huo, Naibu Mrajis wa mahakama Kisiwani Pemba Faraji
Shomari Juma, amesema wamegundua uwepo kesi za familia ikiwemo utelekezaji wa
familia, utoaji wa talaka kiholela pamoja na migogoro ya mirathi.
“Katika mkutano huu tumegundua
changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi miongoni mwa changamoto hizi ni
pamoja migogoro ya kifamilia ikiwemo talaka za mara kwa mara pamoja mirathi, na
wananchi hawajui chakufanya ni nini pindi inapotokea hiyo migogoro lakini
tunashukuru sana ujio wetu huu umeweza kutoa mwanga kwa wananchi hawa na ni
matumaini yetu kuwa wataitumia elimu kwa kutoa taatifa kwa vyombo vya dola na
sheria pindi wanapokumbwa na changamoto mbali mbali za Kisheria” Naibu Mrajis wa mahakama Pemba
Akitoa ufafanuzi juu ya changamoto zinazowakabili wananchi
hao, kadhi wa rufaa Pemba Sheikh Daudi Khamis Salim, amesema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imeweka utaratibu nzuri wa gharama nafuu za ufunguaji wa
kesi ili wananchi waweze kupata haki zao kwa urahisi.
“Ukweli ni kwamba Serikali imeweka gharama nafuu sana za ufunguaji wa kesi katika mahakama ya kadhi ili wananchi waweze kuhimili kufungua kesi na kupata haki zao na niwaase wasiogope na wafike mahakama ya kadhi pindi wanakuwa na migogoro mbali mbali ya kifamilia pamoja na mirathi” Kadhi wa Rufaa Pemba
Mkutano huo maalum baina ya wananchi wa Makoongwe na
watendaji wa mahakama Kisiwani Pemba, ni muendelezo wa mikutano kuelekea kilele
cha maadhimisho ya siku ya sheria Zanzibar.