Waziri wa habari Nape Nnauye amesema serikali imesikitishwa na taarifa iliyotolewa na Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) kuhusu kushindwa kuwasilishwa kwa muswada wa habari bungeni katika bunge la kumi wakati wao walitaraji huenda ungewasilishwa wakati huu bunge likiendelea.
Hata hivyo Nape Nnauye amesema Februari 10, 2023 Muswada wa Huduma ya Habari utawasilishwa bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza huku akiwaomba wadau wa habari kuaminiana.
Nape ametoa kauli hiyo Februari 9, 2023 alipokuwa akizungumza na waandishi wa havari jijini Dodoma.
TAZAMA VIDEO HII HAPA AKIZUNGUMZA WAZIRI NAPE