ZIMWI LA AJALI LAZIDI KUTAWALA BASI LINGINE LAPATA AJALI....

0

 Basi la Kampuni ya Africa Raha limepata ajali katika Kijiji cha Mwibagi barabara ya Mwanza- Musoma wilayani Butiama, Mkoa wa Mara na kusababisha majeruhi.Ajali hiyo imetokea  Jumapili, Februari 12, 2023 saa 9 mchana kwa basi hilo linalofanya safari zake kati ya Musoma, mkoani Mara na Mwanza kupinduka.

Mkuu wa wilaya ya Butiama (DC), Moses Kaegele amesema hadi sasa hakuna vifo ingawa kuna majeruhi ambao wamekimbizwa katika hospitali ya Wilaya ya Bunda kwa matibabu zaidi.

"Majeruhi wamekimbizwa Bunda kwasababau ndipo palikuwa karibu maana ni kama kilomita 21 kutoka eneo la tukio, taarifa zaidi nitatoa baadaye maana hadi sasa bado sijapata taarifa yaani idadi ya majeruhi, chanzo cha ajali na vitu vingine," amesema Kaegele kwa njia ya simu.

USISAHAU KUTEMBELEA CHANNEL HII YOUTUBE
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top