Mkazi wa Kijiji cha Kiperesa, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Sophia Ishuka (56) amejinyonga kwa mtandio akiwa nyumbani kwake kwa madai kuwa mimea yake imeathirika kwa kiwango kikubwa shambani kwake baada ya mvua kukosekana.
Imeelezwa baada ya kufika shambani kwake Machi 19.2023 Bi. Sophia alikuta hali mbaya ya mimea hali iliyompelekea kuanguka ghafla na kupoteza fahamu ambapo baadaye alizinduka na kurejea nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake alieleza majirani zake mkasa na kilichompata akiwa shambani kisha kuingia ndani ya nyumba yake na kujinyonga.
soma zaidi Tanzania web