Aliyelawiti mtoto miaka minne afungwa maisha

0

 Katika kukabiliana na vitendo vya ukatili, Jeshi la Polisi Mkoani Manyara, limefanikiwa kutiwa hatiani watu tisa kwa makosa mbalimbali akiwemo Fadhili Saidi (37) aliyefugwa jela maisha kwa kumlawiti mtoto wa miaka minne.Akizungumza na waandishi wa habari, Machi 16, 2023, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, RPC George Katabazi amesema miongoni mwa waliotiwa hatiani kwa makosa mbalimbali ni pamoja na Fadhili Said (37) amehukumiwa kwenda jela maisha kwa kosa la kumlawiti mtoto mdogo wa miaka minne.

Wengine ni Richard Marting (28) huyu alihukumiwa kwenda jela miaka (30) Mahakama ya Wilaya ya Babati kwa kumbaka binti wa miaka kumi na moja.

Samweli Sylveter (19) alihukumiwa kwenda jela miaka thelathini kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka kumi na sita alisema RPC Katabazi.

Katika hatua hiyo, Kamanda Katabazi aliwataja watu wengine kutoka Wilaya ya Mbulu waliohukumiwa kwenda jela kwa makosa mbalimbali akidai kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano wa wananchi katika kukabiliana na vitendo hivyo.

"Samwel Lulu (43) amehukumiwa kwenda jela miaka thelathini kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka (13), Emmanuel Mollel (21) amehukumiwa kwenda jela miaka thelathini kwa kosa la kumpa mimba mwanafunzi

Mwingine ni Yusuph Ramadhani (34) aliyehukumiwa kwenda jela miaka ishirini kwa kosa la shambulio la kingono kwa mtoto wa miaka minne," alisema RPC Katabazi.

Katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro, RPC Katabazi amewataja watu wengine waliohukumiwa kwenda jela kuwa ni pamoja na Yusuph Fadhili (28) aliyefungwa miaka mitano kwa kosa la shambulio.

"Yusuph fadhili (28) amehukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kumshambulia kijana wa miaka saba, Isaya Daniel (24) amehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kumjeruhi mwanamke wa miaka (31) na Francis Godwin (36) huyu amehukumiwa kifungo cha miezi sita kwa kosa la kumshambulia mke wake," alisema Kamanda Katabazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top