Askari auawa na mpenzi wake kisa wivu wa kimapenzi

0

 Afisa mmoja wa polisi wa kike ameuawa kwa kupigwa risasi na mchumba wake ambaye alikuwa amemtembelea katika kambi yao ya polisi katika wilaya ya Kabale nchini Uganda.


Inaarifiwa kuwa ugomvi ulizuka kati ya jamaa huyo ambaye ni raia na demu wake ambaye ni afisa wa polisi - ugomvi ambao uliishia katika kifo cha afisa huyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, polisi katika Wilaya ya Kabale wameanzisha uchunguzi kuhusu kilichotokea kiasi kwamba polisi huyo wa umri wa miaka 23 kupigwa risasi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, Caroline Komuhangi anayefanya kazi katika kambi ya polisi ya Kabale aliuawa katika nyumba yake ndani ya kambi hiyo.

Rekodi zinaonyesha kuwa mwendazake aliandikisha kuchukua bunduki hiyo kwa zamu ya usiku na kurejea mwendo wa saa kumi na mbili na nusu asubuhi.

Alienda katika nyumba yake ili kupumzika na mpenzi wake kwa jina Denis Arinaitwe akamfuata na ugomvi kuzuka kati ya wawili hao.

"Komuhangi alipojaribu kutoroka, mpenzi wake alichukua bunduki na kumpiga risasi moja mgongoni na mbili kwenye bega na kumuua papo," taarifa ya polisi imesema.

Baada ya kutekeleza mauaji hayo, mwanamume huyo alijaribu kujiua kwa kujipiga risasi kupitia kwa pua lakini akasalia tu na majeraha ya pua.

Maafisa wengine wa polisi ambao walikuwa kambini wamemkamata jamaa huyo na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Kabaale akitarajiwa kukabiliwa na kesi ya mauaji baada ya kutibiwa.
USIKOSE KUTAZAMA VIDEO HII MPAKA TAMATI
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top