Dani Lihawa anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25-31 mkazi wa mtaa wa mizani uliopo kata ya makambako wilayani Njombe amefariki dunia baada ya kupigwa na baadhi ya wananchi mtaani hapo kwa madai ya kwamba ameiba simu.
Shuhuda wa tukio hilo Endrew Omary amesema alikuta baadhi ya watu wanampiga kijana huyo kwa madai ya kwamba ameiba simu ndipo alipolazimika kumpigia simu mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ili kuthibiti tukio hilo.
Aidha Ndugu wa marehemu huyo, Biatus Lihawa amesema wamesikitishwa na tukio hilo na wameiomba serikali kutoa elimu kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi.
Naye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Kelvin Mwangili amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa waliohusika na tukio hilo ni binamu yake marehemu na baadhi ya vijana ambao hajawataja majina kwa sababu za kiuchunguzi.
FAHAMU JINSI YA KUJIAJIRI MTANDAONI KWA KUTAZAMA VIDEO HII