Mama Aachwa na Uchungu Baada ya Muuguzi Kumwibia Mtoto wa Miezi 2

0

 Mwanamke mmoja kutoka Malava katika kaunti ya Kakamega,nchini Kenya ameachwa na uchungu na sintofahamu baada ya kutoweka kwa mwanawe wa miezi miwili katika mazingira tatanishi. 

Mama wa mtoto Abigael Vutabwa (20)

Abigael Vutabwa, 20, anasema mwanawe Cleverton Maraka ametoweka kwa siku nane sasa.

 Masaibu yake yalianza wakati mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia sare ya muuguzi kufika nyumbani kwake, akisema alikuwa akifuatilia chanjo ya Covid-19 katika eneo hilo. 

Vutabwa anasema muuguzi huyo alisema alikuwa akihudumu katika kituo cha afya cha umma eneo hilo na alikuwa ametumwa na serikali kuchukua data za chanjo ya corona. 

Kulingana na Vutabwa, haikuwa mara ya kwanza kwa muuguzi huyo kutembelea nyumba yao kwani siku iliyotangulia, alifika mahali pale lakini hawakusemezana.

 "Nilikuwa nikifua nguo wakati mwanamke huyo aliingia alisema ametumwa na wizara ya Afya kukusanya takwimu za watu waliopokea dozi kamili za Covid," alisema Vutabwa 

 "Niliona begi yake na kumruhusu aingie. Pia nilimpigia simu mama yangu ambaye alimpa maelezo ya chanjo ya familia yetu. Kisha mama yangu akaondoka," aliongeza.

 Baada ya mama yake Vutabwa kuondoka, muuguzi huyo alimuuliza iwapo alikuwa tayari kufanya kazi ya ndani ,Muuguzi huyo alidai kuwa swahiba wake alikuwa amejifungua hivyo alihitaji mfanyakazi. 

Mambo yageuka baada ya kumshika nesi mkono Vutabwa anasema alianza kumshuku alipomsalimia muuguzi huyo kwa mkono.

 "Sijui jinsi mambo yalivyogeuka haraka sana lakini niligundua kuwa kuna kitu hakiko sawa muda si muda akambeba mtoto wangu na tukaelekea mjini." 

“Sijui nilikubali vipi kwenda mjini Kituo chetu cha kwanza kilikuwa Muliro Gardens ambapo alinunua vitafunio na vinywaji, lakini sikuchukua chochote," alisema. 

Wakiwa Muliro Gardens, Vutabwa anasema mwanamke huyo alizungumza na mwanamke mwingine kwenye simu, ambaye alisema ni mfanyakazi mwenzake ambaye alihitaji yaya.

 “Aliniambia muuguzi huyo alikuwa anatusubiri katika Zahanati ya Nabongo. 

Tulipofika pale niliombwa kuketi kwenye sehemu ya kusubiri huku akiongea na mmoja wa wauguzi," alisema.

 Muda si muda, muuguzi alirejea tena na kumuambia Vutabwa kwamba anatakiwa kubadilisha nepi ya mtoto huku wakimsubiri nesi mwingine aliyetaka kijakazi.

 Lakini Vutabwa hakuwa amebeba nepi za ziada hivyo muuguzi huyo alimpa pesa na kumwagiza atafute duka iliyoko karibu na kununua nepi. 

Nesi huyo alijitolea kumbeba mtoto huyo huku Vutabwa akienda dukani kutafuta nepi. 

Vutabwa aliondoka kwenda dukani bila kujua hiyo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kumuoa tena mwanawe. "Niliporudi sikumkuta. 

Watu waliomuona walisema muda mfupi baada yangu kuondoka alipanda pikipiki na kutoroka." 

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Kakamega Joseph Kigen alisema walipokea ripoti hiyo na wanashirikiana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI) kumtafuta mtoto huyo. 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top