Mama awakabili polisi utupu wenyewe wajitia upofu...

0

Wakenya wanazidi kuchambua matukio yaliyoshuhudiwa  katika sehemu mbali mbali wakati wa maandaamano ya muungano wa Azimio la Umoja.

Waandamanaji walinaswa wakishiriki kila namna ya mahanjam katika kuonyesha ufuasi wao kwa kiongozi wa Azimio Raila Odinga. 

Katika tukio moja ambalo limewaacha wengi kinywa wazi, mwandamanaji mmoja wa kike aliamua kushiriki zoezi hilo na suti yake ya kuzaliwa. 

Katika video iliyonakiliwa, mwanamke huyo anaonekana bila nguo kwenye maandamano na hahofii polisi. 

Licha ya polisi kuuma ndimu dhidi ya waandamanaji na kuwarushia vitoa machozi huku wengine wakipokea mijeledi, mama huyo anawaendea polisi bila woga na hadi kupanda juu ya gari lao. 

Ni hali ambao iliwaacha waandamanaji wenzake kwa mshangao mkubwa na kusuburi kuona polisi watafanyaje. 

Hata hivyo, polisi walijipa hamnazo na kumwacha tu kujipa raha juu ya gari lao akiwa utupu  kabisa. Wanamtandao walikuwa na hisia mseto kuhusu kisa hicho baadhi wakisema ilikuwa ni fedheha kwa mama huyo kuvua nguo. 

"Weuh, ata kama ni maandamano hii apana. Kwa nini utoe nguo sasa? Hio ni aibu sana jameni," alisema Dorothy Teckla. Bloga Lemiso Sato naye alisema kilichofanyika ilikuwa athari za kupigwa vitoa machozi siku nzima mpaka ionaingia kwenye ubongo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top