Mama amewaua watoto wake kwa kuwashindisha njaa na kuwaziba pumzi kwa nia ya kuwa 'mashujaa mbele ya Mungu baada ya kifo.
Polisi wa Kenya Jumatano jioni walimkamata Mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie wa kanisa la Good News International kutoka Kilifi kuhusiana na vifo cha watoto hao wawili katika kijiji cha Shakahola.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP),mama huyo ni muumini katika kanisa la mchungaji Mackenzie ambaye yuko chini ya ulinzi wa polisi baada ya mahakama ya Malindi kuamuru kufukuliwa kwa miili ya mtoto hao.
Polisi walifanikiwa kumuokoa mtoto wa tatu, ambaye alisimulia mateso waliyopitia ndugu zake wawili baada ya kushindishwa njaa kwa muda kabla ya mama yao kuwaziba pumzi hadi kufa.
YALIYOTIKISA LEO MITANDAONI👇👇👇