Mwanamke kutoka Long Island nchini Marekani, amemtambulisha mwanamke mwingine ambaye anafanana naye katika ndoa yake yenye doa ili kumzuia mume wake mzinzi kuwanyemelea wanawake wengine.
Kulingana na New York Post, Tehmeena Quintana alikerwa sana wakati mume wake Bryant Quintana alipochepuka miaka mitatu baada yao kuoana na hivyo aliwazia kutatua matatizo yao kwa kujaribu ndoa ya wazi. Kulingana na mke aliyejitolea, Bryant hakuwa mwaminifu kwake hapo zamani pia. "Ninahisi kwamba ikiwa uko na mwanamume, unapaswa kufanya chochote kinachohitajika kusimamisha ndoa yakeo," alisema.
“Nataka kuishi maisha yangu yote naye. Chochote anachotaka, chochote kinachomfurahisha, nitampa," aliongeza. Tehmeena aliamua kutumia mitandao ya kijamii kumtafuta mtu anayefanana naye ili kuingia katika ndoa ya mtaala.
"Nilijua kwamba ingeweka akili za Bryant hapa. Ni sawa kusema nilitafuta msichana anayefanana nami kwa sababu Bryant anapenda hivyo," alisema.