MOI yapokea majeruhi 280 wa bodaboda kwa mwezi

0

 Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imekiri kupokea majeruhi wa ajali za bodaboda wastani wa watu 9 hadi 10 kwa siku ambapo ni sawa na 70 kwa wiki na 280 kwa mwezi.


Akizungumza  jijini Dar es Salaam kwenye mafunzo ya kimataifa ya matumizi ya mashine za upasuaji yaliyoandaliwa na Taasisi ya MOI na Chuo Kikuu cha Weill Cornell Medicine cha New York nchini Marekani, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk Respicious Boniface amesema kuna ongezeko la ajali hususan za pikipiki ambazo zinasababishwa na kutofuatwa kwa sheria za barabarani ambapo wahanga wengi hawavai kofia ngumu (Helment).

“Kuna ongezeko la ajali kwa asilimia 5 hadi 6 kwa mwaka ambapo kwa siku tunapata majeruhi wa ajali za barabarani 10 hadi 15 kati ya hao 10 ni bodaboda kwa mwezi ni 350 hadi 400 ambao wa bodaboda ni 280,” amesema Respicious.

Daktari Bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu kutoka MOI, Dk Hamis Kimaro amebainisha kuwa wagonjwa wengi wa upasuaji walioumia vichwa, mgongo wanatokana na ajali za barabarani ambao wanachukua robo tatu ya wagonjwa wote wa upasuaji.

“Changamoto kubwa tunayoipata kwa wagonjwa wa majeruhi wa ajali wengi wakija hawana ndugu wa kuwahudumia, hawana kadi ya bima hawana hela mfukoni, hii imekuwa changamoto kwa sababu ni zaidi ya asilimia 75 na taasisi ndiyo inayoingia gharama za kuwahudumia,” Dk Kimaro.

Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka Chuo kikuu kishiriki cha MOI, Dk Victor Meza amesema imekuwa ni muhimu kwa wao kupata ujuzi huo ambapo yatafanyika kwa siku tano, mbili zikiwa za darasani na tatu zikiwa za vitendo kwani watapata elimu na uzoefu wa kutosha kuweza kuwahudumia wahitaji wa upasuaji ambao wengi wao wanatokana na ajali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top