Mume ampiga mchungaji kwa madai mkewe amekuwa akimpelekea chakula chake

0

 Mwanamume mmoja ameishangaza mahakama ya Mombasa baada ya kutoa malalamishi yake kwamba mkewe alimuambukiza ukimwi na pia anachukua chakula chote anachonunua yeye na kukipeleka kwa mchungaji kanisani.

“Ni mke wangu na aliniambukiza HIV. Nikinunua chakula, anakipeleka chote kwa mchungaji na anafanya hivi kila siku. Mchungaji pia alimnunulia simu,” mwanamume huyo alisimulia kwa uchungu.

Mwanamume huyo aliiambia mahakama baada ya kufikishwa pale kama mtuhumiwa wa kumshambulia mchungaji wa kanisa moja.

Mwanamume huyo alifikishwa mahakamani siku chache zilizopita akishtakiwa kwa kosa la kumshambulia mchungaji, na safari hii baada ya kukubali makossa yake, aliamua kuishangaza mahakama kwa kusimulia kilichompelekea kumshambulia mtumishi wa Mungu.

“Ndiyo ni kweli nilimpiga,” alisema mshukiwa akieleza ni kwa nini alishindwa kujizuia na kumvamia pasta.

Alieleza kuwa siku hiyo majira ya saa tano asubuhi alikwenda katika kanisa hilo lililoko Mombasa kumuuliza mchungaji kwa nini mkewe amechukua muda mrefu katika kanisa lake.

Mshukiwa huyo alipofika kanisani, alimwendea pasta kwa ajili ya mazungumzo, lakini mtumishi akamsukuma.

“Nilikereka na kumpiga kofi shingoni kwa sababu alinikosea heshima huku mke wangu akienda kanisani kwake na watoto bila sababu za msingi,” alieleza.

Baada ya kumzaba kofi, mchungaji alianguka chini na kupiga kelele ambapo watu walifika na kuwatawanyisha. Baadae aliarifiwa kwamba mchungaji amemfungulia kesi.

Kulingana na pasta, mshukiwa alimpiga mara kadhaa huku marafiki zake wakitazama.

“Nilipiga kelele lakini kabla waokoaji hawajafika, alinipiga mweleka chini ya mteremko. Nilijeruhiwa kwenye mkono wangu wa kulia kati ya kidole cha shahada na kidole gumba. Majirani walikuja kuniokoa lakini mshukiwa alisisitiza kunifundisha somo la kutotoa kimbilio kwa wake za watu,” alisema.

Hakimu aliamuru ripoti za tathmini ya kabla ya hukumu na mwathiriwa kabla ya kumhukumu mshukiwa.

Kesi hiyo itatajwa Aprili 5.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top