MVEKA JELA KWA KUMKATA MGAMBO KOROMOE

0

 Mahakama kuu kanda ya Iringa iliyoketi wilaya ya Mufindi imemuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa Mkazi wa kijiji cha ugenza Wilaya ya Mufindi, Chesco Mveka (49) baada ya kukutwa na hatia ya kosa la mauaji ya Silayo Mbwimbije ambaye alikuwa ni mgambo wa kijiji kwa kukamta koromeo lake.


Shauri hilo la mauaji namba 19/2016 ambalo hukumu yake imetolewa jana Jumatano Machi 22, 2023 katika mahakama kuu kanda ya iringa ambayo imeketi wilayani Mufindi.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya iringa Ilvin Mgeta amesema kuwa mahakama hiyo imemtia hatini mshtakiwa Chesco kwa kutenda kosa la mauaji ya Silayo

Aidha Jaji Mgeta amesema mshtakiwa huyo amehukumiwa chini ya kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la mwaka 2022 ambapo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa chini ya kifungu namba 197 cha kanuni ya adhabu rejeo 2016.

Jaji Mgeta amesema kifungu hicho kinatoa aina Moja ya adhabu ambayo ni kunyongwa hadi kufa kwa mshtakiwa ambaye anapatika na hatia ya kosa kama hilo.

Mgeta amedai kuwa ushaidi ulitolewa mahakamani hapo umeonyesha mshtakiwa huyo ndiye ametenda kosa hilo akiwa na nia ovu ya kusababisha kifo.

Akisoma maleezo hayo ,Jaji Mgeta amesema kuwa inadiwa kuwa Aprili 3, 2013 katika kijiji cha ugenza Wilaya ya Mufindi,aliuwawa mtu ambaye anaitwa Silayo Mbwimbije, ambapo mshtakiwa alipoulizwa kuhusu tukio hilo alikana kutenda kosa hilo.

Awali akitoa maeleezo kabla ya hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa serikali Yahaya Misango ameiomba mahakama kuzingatia kifungu 197 kama kinavyoelekeza kuhusu mshtakiwa ambaye anapatika na hatia ya kosa kama hilo.

Kwa upande wa utetezi wakili Msomi Lazaro Hukumu amesema baada ya mteja wake kukutwa na hatia hakuwa na ombi kwa mahakama kwa kuzingatia kosa halina adhabu mbadala.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top