Mwanafunzi afia nyumbani kwa mpenzi wake

0

 Emmanuel Kayuni (21) mwanafunzi katika shule ya Mansa, amefariki akiwa nyumbani kwa mpenzi wake katika mji wa Ndola alikokwenda baada ya kutoroka shule huku wazazi wake wakijua anaendelea na masomo, tovuti ya Zambian observer imeripoti.Baba mzazi wa marehemu aitwaye John Kayuni, alisema mtoto wake alirudi kutoka shule kukutana na Princess Mwaba mwenye umri wa miaka 20 ambapo umauti ukamkuta.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Ukanda wa Shaba, Peacewell Mweemba alisema tukio hilo lilitokea Jumatano saa 09:00 mchana katika eneo la Northrise.

“Mnamo Machi 21, marehemu na Princess Mwaba walikwenda kwenye nyumba ya kulala wageni huko Northrise ambapo walilala usiku mmoja na alikuwa akilalamika kuwa ana shida ya moyo, asubuhi waliondoka hadi kwenye nyumba yao iliyoko Northrise ambapo marehemu alienda kununua nyanya sokoni,” amesema Mweemba.

Anaendelea kusema aliporejea alianguka kwenye mlango ambapo Princess na baba mwenye nyumba walijaribu kumkimbiza Emmanuel katika Hospitali ya Teaching ya Ndola (NTH) lakini madaktari wakasema kuwa alikuwa ameshafariki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top