Mtoto mchanga mwenye umri wa siku mbili, amenusurika kufa ,baada ya kutupwa chooni na mama yake mzazi, mara baada ya kuzaliwa katika kijiji cha Uruwila, kilichopo Halmashauri ya Nsimbo ,wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, huku chanzo kikidaiwa kuwa ni hali ngumu ya maisha ya mama huyo baada ya kukataliwa na baba wa mtoto.
Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Dk. Maria Matei amethibitisha kumpokea mtoto huyo na asema alikuwa na majeraha usoni na mikononi lakini anaendelea vizuri huku wananchi wakilaani kitendo hicho.
Mama wa mtoto huyo bado hajapatikana