Ndugu wawili wapigwa na radi wakivua samaki

0

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limewata wavuvi kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua baada ya wavuvi wawili ndugu kupigwa radi na kusababisha kifo chao Machi 19 katika Kijiji cha Mtandi, Kata ya Msimbati, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.


Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa tukio hilo lilishuhudiwa na wavuvi wenzao waliokuwa wakivua katika eneo hilo.

Katembe aliwataja marehemu hao kuwa ni Shani Salum Yusuph (53) na Nangomwa Salum Yusuph (58) wavuvi wote wakazi wa Kijiji cha Mtandi.


“Siku ya tukio saa 4 asubuhi marehemu hao ambapo ni ndugu walienda baharini wakiwa na mtumbwi ambao haujasajiliwa namba na kuingia baharini kwa lengo la kuvua wakiwa wanavua mvua kubwa ilianza kunyesha ndipo walipopigwa na radi na kufariki ambapo tukio hilo lilishuhudiwa na wavuvi wenzao ambao walitoa taarifa kwa Polisi,” amesema.

“Juhudi zilifanyika na kuwea kuichukua mili ya marahemu na kuiweka ufukweni ambapo kwa mujibu wa majibu ya daktari ilionyesha kuwa vifo hivyo vilitokana na kupigwa radi,” alisema Katembo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top