Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemshukuru Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris kwa kukubali mwaliko wake wa kuja Tanzania ambapo amesema Watanzania sasa wanamsubiri Rais Joe Biden aitembelee Tanzania na amemuomba Kamala amfikishie salamu na mwaliko Biden na amwambie Tanzania inamsubiri.
Akiongea Ikulu Dar es salaam leo mbele ya Kamala Harris, Rais Samia amesema “Hii ni hamasa kubwa na ushuhuda kwa Wanawake wa Kitanzania kuona Wanawake wawili, Rais wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Marekani wanakutana pamoja tena katika Mwezi ambao tumeadhimisha siku ya Wanawake”
“Ninakushukuru Dada yangu Mpendwa Kamala kwa kupokea mwaliko wangu, ziara yako inathibitisha uwepo wa mahusiano ya Nchi zetu katika maeneo mbalimbali, kwa ziara yako nina uhakika sasa Watanzania wanamsubiri Rais Joe Biden kuitembelea Tanzania, naomba umfikishie salamu zangu kwake na mwaliko na umwambie Tanzania inamsubiri Joe Biden”
“Karibu Tanzania, nategemea unafahamu baadhi ya maneno ya Kiswahili mfano neno karibu, jambo na safari, suala la demokrasia limekuwa muhimu sana kwenye Serikali yangu, namshukuru Joe Biden kwa kunialika kushiriki mkutano wa demokrasia mwaliko huo unaonesha Marekani inatambua mchango wetu kwenye demokrasia, ni imani yetu ziara hii itakuwa jukwaa la kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano”
TAZAMA FULL VIDEO WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
Serikali ya Marekani imesema kuwa itaendelea na katika Mpango wa Dharura wa Rais wa nchi hiyo wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania, ambapo Marekani inapanga kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 433 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 995 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Tanzania ni mojawapo ya nchi 12 zinazoshiriki katika Muungano wa Kimataifa Kutokomeza UKIMWI kwa
Watoto, muungano unaoongozwa na Shirika ya UKIMWI la Umoja wa Mataifa
(UNAIDS) na Ofisi ya Mratibu wa Shughuli za Kupambana na UKIMWI Kimataifa.
Kwa ubia na Serikali ya Tanzania, PEPFAR inasaidia kuandaliwa kwa sera za afya
zitakazoimarisha programu na afua za VVU kwa watoto. Aidha, PEPFAR inaisaidia Tanzania kuweka sera za afya zitakazoimarisha afua dhidi ya VVU zinazowalenga Watoto.
amesema kwamba katika maombi yake ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024, utawala wa Biden-Harris umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 sawa na Shilingi Bilioni 37 za Tanzania ili kugharamia programu zinazohusu demokrasia, haki na utawala bora nchini Tanzania.