Sita mbaroni kwa mauaji, kufukua makaburi

0

 Watu sita wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya mauaji ya watu, kufukua makaburi wilayani Manyoni na kuchukua sehemu za siri za miwili ya watu waliozikwa kwa ajili ya kutengeneza dawa ya kupata utajiri kuwauzia wateja wao.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stella Mutabihirwa, katika taarifa yake Jana kwa vyombo habari, alisema watuhumiwa hao ambao hakuwataja majina kwa kuwa uchunguzi bado unaendelea, walikamatwa kufuatia msako uliofanywa na jeshi hilo kuanzia Machi 16 hadi 24 mwaka huu katika maeneo mbalimbali wilayani Manyoni na vijiji jirani vya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Alisema watuhumiwa hao baada ya kukamatwa na kuhojiwa walikiri kuhusika na mauaji ya mtu mmoja mwanaume ambaye hajafahamika jina lake mwenye umri kati ya miaka 40 na 45 yaliyotokea Machi 3 mwaka huu eneo la relini Manyoni huku kifo chake ikisadikiwa kilitokana na kukanyagwa na treni kichwani na mguu wa kushoto.

Kamanda Mutabihirwa alisema baadhi ya viungo vya mtu huyo vilikuwa pembeni ya kiwiliwili katika njia ya treni huku viungo vya sehemu y Siri vikiwa vimenyofolewa.

"Tulivyowahoji watuhumiwa walikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kwamba walikata sehemu za siri kama nywele,kuchapa na ulimi kwa lengo la kutengeneza dawa ili kuwapatia wateja wao wanaohitaji utajiri," alisema.

Aliongeza kuwa watuhumiwa hao pia wamekiri kujihusisha na vitendo vya kufukua makaburi wilayani Manyoni na kuua watu kwa lengo la kupata sehemu za viungo vya binadamu kwa ajili ya kutengeneza dawa ya kupata utajiri.

"Katika kukamilisha upelelezi wetu Jeshi la Polisi lilifanya upekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa mmoja wao na kufanikiwa kukuta suruali moja nyeusi ya marehemu aliyeuawa Machi 3, 2023,vibuyu viwili vyenye shanga, kibuyu kimoja chenye ngozi ya kondoo," alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 


 

 




#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top